Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Rex Tillerson akiwa nchini Kenya katika Ziara yake ya siku nane ya kuzitembelea nchi tano za Afrika ameugua gafla kutokana na hali yake kiafya kutokuwa nzuri.
Hivyo ameamua kusitisha baadhi ya shughuli alizokuwa anapaswa kufanya nchini Kenya.
Ambapo Maofisa wamesema watahairisha baadhi ya ratiba ambazo Tillerson alikuwa ameweka ikiwa ni pamoja na safari yake ya kwenda kuona eneo ambalo ubalozi wa Marekani ulikuwa umelipuliwa mwaka 1998.
Msemaji wake amesema,Tillerson amekuwa kwenye ratiba ngumu katika ziara yake ya Afrika wakati huo huo akitumia muda mwingi kwenye mazungumzo ya simu kufuatilia kazi nyingine nchini mwake kama vile suala la Korea Kaskazini.
-
Tillerson awapongeza Uhuru Kenyatta na Raila Odinga
-
Tillerson atofautiana msimsmo na Trump kuhusu Afrika
Waziri huyo amefanya ziara hiyo kwa lengo la Kutafuta ushirikiano katika kupambana na ugaidi, uongozi bora, Uimarishaji wa amani na usalama, Kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji.
Rex Tillerson kiongozi mwenye umri wa miaka 65 ambaye anafanya ziara hiyo barani Afrika ikiwa ni mara yake ya Kwanza kuzulu Afrika ambapo Wizara yake ya mambo ya nje imetaja nchi tano ambazo atazuru ikiwa ni Kenya, Ethiopia, Djibouti, Chad na Nigeria.
Kenya ikiwa ni nchi ya pili kutembelea ambapo alianza na Ethiopia huku zikiwa zimesalia nchi tatu, na ziara hiyo imetajwa kukamilika tarehe 13, Machi mwaka huu.