Timu ya mgombea wa Republican, Donald Trump imeendelea kumshambulia Papa Francis kufuatia kauli yake ya kuhoji ukristo wa mgombea huyo aliyetaka kujenga ukuta kati ya Mexico na Marekani ili kuzuia wahamiaji.

Papa Francis alieleza kushangazwa na kauli ya Trump kutaka kujenga ukuta kati ya nchi hizo badala ya kuwaza kujenga daraja na kueleza kuwa mtu anayefanya uamuzi huo hadhani kama ni Mkristo.

Moja kati ya wapambe wa karibu wa Donald Trump, anayefahamika kwa jina la Susan DeLemus ameandika kupitia Facebook kuwa kiongozi huyo mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, ni ‘mpinga Kristo’.

“Papa ni mpinga Kristo. Fanya utafiti wako,” DeLemus alimjibu moja kati ya wafuasi wake kwenye mtandao wa Facebook aliyetaka kujua mtazamo wake kuhusu kauli ra Papa Francis kwa Trump.

“Sina uhakika Papa ana nani kweli ndani ya moyo wake,” aliongeza DeLemus

Hata hivyo, DeLemus alipofanya mahojiano baadae na POLITICO, alieleza kuwa alizungumzia Papa kama nafasi au cheo kwa kumuita mpinga Kristo kwa kuwa aliwahi kuwepo Papa mmoja katika historia aliyetajwa kama mpinga Kristo, na kwamba yeye hakumuongelea moja kwa moja Papa kama mtu bali nafasi.

“So that’s all I was referring to, the papacy, not particularly that one particular pope because the papacy is a seat. It’s not just one person.”

 

Sekta ya afya kupewa bei elekezi, Mlima wawekwa Kuingia Muhimbili
Profesa Lipumba ataka Magufuli atangaze mshahara wake, ajikate kusaidia