Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja amewatahadharisha Wananchi wa Mkoa wa Iringa kuacha kutembea usiku, ili kuepukana na madhara ya kuvamiwa na Simba walioingia katika makazi ya watu.

Masanja ameyasema hayo Bungeni jijini Dodoma na kuongeza kuwa Serikali itaendelea kutoa elimu kuhusu jambo hilo na kwamba tayari wamepeleka usaidizi ili kuhakikisha Simba hao wanarejea katika makazi yao.

Amesema, “niendelee kutoa elimu kupitia Bunge hili kwamba wakati huu ambapo tunawasaka hawa Simba wananchi wawe na tahadhari ya kutotembea usiku lakini pia wenye mifugo wawashe mioto kuzunguka maeneo ya mifugo ili kuepusha Simba wasisogee katika maeneo yao.”

Aidha, Masanja amesema Serikali tayari imeshapeleka helikopta inayozunguka usiku na mchana kuhakikisha Simba hao wanapatikana na kurudishwa katika maeneo yao ili kuhakikisha maisha ya Watanzania yanalindwa kwa gharama yoyote.

Mikel Arteta: Tutasajili kikosi bora, imara
Meshack akutana na siku ya 40 wizi wa misalaba Makaburini