Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania – TMA, imetoa tahadhari ya uwepo mvua kubwa zinazotarajiwa kunyesha kwa siku mbili mfululizo kuanzia hii leo Machi 14 na 15, 2023.
Taarifa hiyo iliyotolewa na TMA imeeleza kuwa Machi 14, 2023 Mikoa itakayopata mvua kubwa ni Iringa, Mbeya, Songwe, Njombe, Rukwa, Katavi, Tabora, Kigoma, Singida, Dodoma na Ruvuma.
Aidha, kwa Machi 15, 2023, Mikoa itakayopata mvua kubwa ni Mara, Simiyu, Shinyanga, Mwanza, Iringa, Mbeya, Songwe, Njombe, Rukwa, Katavi, Tabora, Kigoma, Singida, Dodoma na Ruvuma.
Kutokana na tahadhari hiyo, TMA imewashauriwa Wananchi kuchukua tahadhari mapema kutokana na athari zinazoweza kujitokeza kwa baadhi ya maeneo kuzungukwa na maji pamoja na ucheleweshwaji wa shughuli za uchumi na usafirishaji.