Mamlaka ya hali ya hewa nchini,(TMA), imetoa muelekeo wa mvua za msimu za mwezi Novemba 2020 hadi April 2021 ambapo imeeleza uwepo wa mvua za wastani katika nyanda za magharibi Na mvua za wastani hadi wa chini kwa upande wa magharibi.

Akitoa maelezo katika mkutano na waandishi wa habari leo, kuhusiana na utabiri huo Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk.Agness Kijazi, amesema kuwa mvua hizo zinatarajiwa kuanza mwezi wa Novemba na kuisha katika mwezi wa nne huku muda wa kuanza mvua hizo unatofautiana kulingana na maeneo husika.

Aidha imewatahadharisha  wakazi waliopo maeneo hatarishi  kuchukua tahadhari ilikuepukana na athari zinazoweza kujitokeza kufuatia mvua hizo za msimu.

“Vipindi vya mvua kubwa vinaweza kusababisha kutuama kwa maji na mafuriko na kupelekea uharibifu wa miundombinu na upotevu wa maisha na mali,mamlaka za miji na wadau wengine wanashauriwa kuboresha mifumo ya kupitisha maji taka na kuisimamia ili kupunguza athari zinazoweza sababisha mafuriko,”amesema Kijazi.

Mamlaka hiyo imetoa tahadhari kwa wavuvi na mamlaka za miji juu ya athari zinazoweza kujitokeza katika msimu wa mvua unaotarajiwa kuanza kuanzia mwezi Novemba 2020.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Oktoba 22, 2020
Kaze: Viungo wanaiangusha Young Africans