Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA) imesema itakuwa na ongezeko la joto katika baadhi ya maeneo nchi kufuatia kuwepo kwa hali ya unyevunyevu angani.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na mkurugenzi mkuu TMA Agnes Kijazi ambayo imeeleza kwa kawaida kipindi cha octoba hadi march kila mwaka jua la utosi linakuwa katika kizio cha kusini mwa dunia.
Taarifa hiyo imeeleza kwamba Tanzania ikiwa ni moja ya nchi zilizopo katika kizio cha kusini huwa na hali ya joto kali katika maeneo mengi ikilinganishwa na maeneo mengine.
”Hapa nchini vipindi vya jua la utosi vinafikia kati ya mwisho mwa novemba wakati jua la utosi likiwa linaelekea kusini ( Tropiki ya kaprikoni) na hali hiyo hujirudia tena wakati jua la uosi likiwa linaelekea kaskazini (Tropiki ya kansa)” ilieleza taarifa hiyo
Aidha mikoa ambayo itaathirika zaidi ni ukanda wa pwani yanayotarajiwa kuwa na kiwango cha juu cha joto cha nyuzi joto 32 hadi 34 hususan kwa maeneo ya Dar es salaam, Tanga, unguja na Pemba.