Mamlaka ya Hali ya hewa Tanzania TMA imetoa angalizo la mvua kubwa leo Tarehe 23/02/2022 kwa maeneo machache ya mikoa ya Songwe, Mbeya, Njombe, Iringa, Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Morogoro, Ruvuma, Lindi na Mtwara.

Pia imetoa angalizo la upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita 2.0 kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani ya bahari ya Hindi (mikoa ya Lindi, Mtwara, Tanga, Dar es Salaam na Pwani

Aidha, TMA imeongeza kuwa mvua itaendelea kunyesha kwa siku mbili zijazo kwa baadhi ya mikoa nchini Tanzania.

Balozi Mbarouk amuaga Balozi wa Vatican
Polisi apigwa mawe na kichaa hadi kufa