Mamlaka ya hali ya hewa iliyopo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano nchini Tanzania imewatahadharisha wananchi kuwepo kwa hali mbaya ya hewa katika maeneo yote ya pwani kuanzia leo usiku.
Hayo yamebainishwa na taarifa zilizotolewa na mamlaka hiyo jioni ya leo (Jumapili) na kudai kutakuwepo vipindi vifupi vya mvua kubwa ambazo zinatarajiwa kunyesha katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Mwanza, Mara, Simiyu, Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Morogoro, Dar es Salaam, Pwani, Tanga pamoja na visiwa vya unguja na Pemba.
Hata hivyo, TMA imesema kuwa kutakuwepo upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayozidi mita 2 ambavyo vinatarajiwa katika ukanda wote wa Pwani.