Tanzania Media Foundation (TMF) imesema kuwa iko tayari kulipia gharama zote za matangazo ya vikao vya Bunge kurushwa moja kwa moja kupitia Kituo cha runinga cha TBC1.

Ahadi hiyo imetolewa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa TMF, Ernest Sungura alipokutana na wamiliki wa vyombo vya habari, wahariri na waandishi wa habari kwa ujumla. Kikao kilichohudhuriwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Asha Mwambene akimuwakilisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye.

Mkurugenzi wa TMF, Ernest Sungura

Mkurugenzi wa TMF, Ernest Sungura

Sungura alieleza kuwa TMF iko tayari kulipia gharama hizo ili kusaidia Serikali kuvuka kikwazo hicho, kwani Wananchi wana haki ya kuangalia Wawakilishi wao wanawaeleza nini.

Kwa mujibu wa Taarifa zilizotolewa Bungeni na Serikali, huigharimu zaidi ya shilingi bilioni 4.2 kurusha matangazo yote ya vikao vya Bunge moja kwa moja kupitia TBC1. Hali iliyopelekea wao kuamua kurusha ‘Live’ baadhi ya vikao, na vingine kurushwa usiku baada ya kurekodiwa na kuhaririwa.

Katika hatua nyingine, Mkurugenzi huyo wa TMF, alieleza kuwa watahisani hatua ya ukusanyaji wa maoni ya wadau ili yaweze kuingizwa kwenye muswada wa Sheria Mpya kabla haujawasilishwa Bungeni.

Mwambene akiongea kwa niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, alieleza kuwa serikali inaendelea kuwashirikisha wadau na kukusanya maoni yao kuhusu muswada huo wa sheria.

“Bado tuko kwenye hatua ya mchakato wa kupokea maoni ya wadau, ninaamini kwamba sheria itakayopitishwa itaakisi maslahi yao pia,” Mwambene anakaririwa.

Pia aliwapongeza TMF kwa kuendelea kuvipa vyombo vya habari misaada ya kifedha kwa lengo la kuimarisha taaluma ya habari nchini.

 

 

Bashe aitahadharisha Elimu Bure ya Magufuli
Hadji Manara: TFF Msipioamua, Tutaamua Sisi