Uongozi wa klabu ya West Bromwich Albion umesitisha mkataba wa meneja Tony Pulis, kufuatia matokeo mabovu yanayoendelea kuwaandama katika ligi kuu ya England msimu huu.

Mwishoni mwa juma lililopita West Bromwich Albion walikubali kufungwa mabao manne kwa sifuri dhidi ya mabingwa watetezi Chelsea.

Kisago hicho kimekua chanzo cha kufukuzwa kazi kwa Tonny Pulis, ambaye ameonekana hana njia mbadala ya kuinusuri West Brom inayoshuka nafasi ya 17 kwenye msimamo wa ligi ya PL, kwa kufikisha point 10.

Meneja msaidizi Gary Megson, ameteuliwa kuwa meneja wa muda hadi uongozi utakapomtangaza meneja mpya atakaechukua nafasi ya Pulis.

Mwenyekiti wa klabu hiyo John Williams ameviambia vyombo vya habari kuwa, uamuzi huo umefikia kwa kuzingatia maslahi ya klabu.

“Tuko katika biashara ya kupata matokeo mazuri, lakini kutokana na matokeo mabaya ambayo yamekuwa yakishuhudiwa kufikia mwishoni mwa msimu uliopita na kufikia sasa matokeo yamekuwa mabaya.” Alisema Megson.

Mwishoni mwa juma hili West Brom watakutana na Tottenham kwenye uwanja wa Wembley.

Magazeti ya Tanzania leo Novemba 21, 2017
Magazeti ya Tanzania leo Novemba 20, 2017