Ndoto za mshambuliaji Saido Berahino za kuitumikia klabu ya Tottenham Hotspurs ziliingia gizani dakika za mwisho hapo jana baada ya uongozi wa klabu yake ya West Brom kuitakaa ofa iliyotumwa kutoka kaskazini mwa jijini London.

Spurs walijaribu kutuma ofa kwa mara ya nne mfululizo kwa kuongeza dau la paund million 5 kwa kuamini huenda ingekubaliwa, lakini mambo yalienda tofauti na kutambua fika hawawezi kumsajili mshambuliaji huyo mzaliwa wa nchini Burundi.

Spurs walikua wakijaribu kumsajili Berahino mara kwa mara na mara ya mwisho waliwasilisha ofa ya paund million 20, ambayo ilikataliwa kwa kuwekewa vikwazo na meneja wa West Brom, Tonny Pulis.

Kwa mantiki hiyo sasa Saido ataendelea kubaki kwenye kikosi cha West Brom na kuutumikia mkataba wake kama unavyoagiza na harakati za usajili wake huenda zikaibuliwa tena mwanzoni mwa mwaka ujao, ama mwishoni mwa msimu huu.

Berahino amekua kivutio katika uchezaji wake kutokana na juhudi anazozionyesha uwanjani kwa kuisaidia West Brom kwenye safu ya ushambuliaji kwa kufunga mabao muhimu ambayo yamekua yakiisaidia klabu hiyo katika mpango wa kusaka point tatu.

Hali Tete kwa Twiga Stars
Lennon Achukuliwa Jumla Goodson Park