Timu ya Township Rollers ya Botswana imesema inawafahamu vizuri wapinzani wao Yanga ambao watakutana kesho kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa Afrika.
Mabingwa hao wa Botswana watashuka katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam kesho kucheza na Yanga mchezo wa hatua ya kwanza ya michuano hiyo.
Kocha mkuu wa timu hiyo, Nicola Kovazovic amesema mchezo utakuwa mgumu kutokana na kucheza mechi siku tatu zilizopita na kusafiri kuja nchini.
Kovazovic amesema wachezaji wake wana presha kubwa kuelekea mchezo huo lakini watajitahidi kupata ushindi ili iwe rahisi kwenye mechi ya marudiano nchini Botswana.
-
Video: Deontay Wilder amshikisha adabu Ortiz, amvimbia Anthony Joshua
-
Pacquiao atosa pambano la promota, ‘ni kama unanitusi’
“Kila kitu ambacho nilitakiwa kukijua kuhusu Yanga nakijua mpaka sasa, tunaamini mchezo utakuwa mgumu lakini tumejiandaa kushinda,” alisema Kovazovic.
Mchezo huo utaanza saa 10:30 jioni huku maandalizi yote yakiwa yamekamilika.