Serikali imesema kutakuwa na ongezeko la tozo ya michezo ya kubahatisha kutoka Sh 10,000 hadi Sh 30,000 kwa kila mashine ya sloti katika maeneo ya baa.

Aidha, itaanza kutoza tozo ya asilimia 1.5 kwa vifaa vinavyotumika kuzalisha, kusambaza, kudurufu na kutunza kazi za sanaa, uandishi na ubunifu mwingine ukiwemo wa muziki, filamu, vitabu, picha na aina nyingine za kazi za ubunifu.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba alibainisha hayo jana bungeni Dodoma wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya serikali kwa Mwaka wa Fedha wa 2023/2024.

Alisema kuwa, serikali pia itaanzisha ada ya maombi ya Sh 500,000 na ada ya leseni kuu ya Dola za Marekani 10,000 kwa mwaka kwa mashine za sloti kwenye maduka na baa.

Nyingine ni ada ya maombi ya Sh 500,000 na ada ya leseni kuu ya Dola za Marekani 5,000 kwa mwaka kwenye mashine arobaini za sloti.

Kwa mujibu wa Dk Mwigulu, lengo la hatua hii ni kuweka tofauti kati ya shughuli za mashine za sloti katika maeneo ya baa, maduka na shughuli za mashine arobaini za sloti na kuwezesha ufanisi na udhibiti bora wa michezo ya kubahatisha nchini.

Aidha, hatua hiyo inalenga kupunguza kiwango cha kodi kutoka asilimia 25 hadi asilimia 18 katika mapatoghafi ya michezo ya kubahatisha kwenye maeneo ya uendeshaji wa mashine arobaini za sloti.

Lengo la hatua hii ni kuleta usawa katika utozaji kodi katika michezo ya kubahatisha inayoshabihiana.

Alipendekeza marekebisho katika sheria ya michezo ya kubahatisha ikiwemo kuanzisha michezo ya meza isiyozidi miwili katika maeneo yenye mashine za sloti arobaini.

“Hatua hii inatarajiwa kuongeza mapato ya seri- kali kwa Sh milioni 4,223 katika Mwaka wa Fedha wa 2023/24,” alisema.

Alipendekeza kutoza ushuru wa bidhaa kwa kiwango cha asilimia 20 kwenye mashine za Kamari zinazoingizwa kutoka nje ya nchi na zinazozalishwa nchini.

Lengo la hatua hii ni kuongeza mapato ya serikali na inatarajiwa kuongeza mapato ya Sh milioni 1,365.4.

Dk Mwigulu alisema serikali itaanza kutoza tozo ya asilimia 1.5 katika vifaa vya sanaa vikiwemo vinyl, mini disc, compact disc, DVD na SD memory.

Nafuu gharama za umilikishaji Ardhi wapiga hodi
Chongolo avunja ukimya sakata la mkataba DMP