Kikosi cha  TP Mazembe, leo kinakamata pipa kuanza safari ya kwenda nchini Japan.

Watanzania wawili, Mbwana Samatta na mshkaji wake, Thomas Ulimwengu watakuwa sehemu ya msafara huo wa mabingwa hao wa Afrika kwenda kucheza michuano ya Kombe la Dunia kwa klabu.

Ulimwengu amezungumza  kutoka Lubumbashi na kusema:

“Tunaondoka kesho (leo), mimi pia nipo vizuri. Kweli niliumia kidogo lakini nimepata matibabu na sasa niko vizuri.”

Wawili hao wanaendelea kuweka rekodi kwa mara nyingine ya kuwa Watanzania wa kwanza kucheza michuano ya Kombe la Dunia kwa klabu.

Mazembe ya DR Congo, inacheza michuano hiyo baada ya kubeba ubingwa wa Afrika kwa kuifundisha kazi USM Alger ya Algeria kwa kuifunga mechi zote mbili za nyumbani na ugenini.

Podolski Akutana Uso Kwa Macho Na Mayweather
Kuelekea Disemba 12, Yanga Bado Hakijaeleweka