Mechi ya kuunganisha mataji ya soka barani, maarufu Super Cup ya CAF itafanyika kati ya Februari 19 na 21, mwakani mjini Lubumbashi.

Taarifa ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) imesema kwamba hakutakuwa na mabadiliko yoyote ya tarehe juu ya mchezo huo mmoja kwa mwaka.

Super Cup ya CAF inatarajiwa kuchezwa wikiendi ya ya Februari 19 hadi 21 mwaka 2016 nyumbani kwa mshindi wa taji la Ligi ya Mabingwa, ambaye ni TP Mazembe ya DRC dhidi ya Etoile Sportive du Sahel ya Tunisia, washindi wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Arsene Wenger Na Arsenal Yake Kujihukumu Leo
Mourinho Na Bosi Wake Wabumba Jambo Chelsea