Kamisheni ya Kusimamia Ngumi za Kulipwa Tanzania ‘TPBRC’ imetoa pongezi kwa mabondia walioshinda ubingwa ndani na nje ya nchi kati ya tarehe 28 na 29 Oktoba-2023.
Mapambano yaliyounguruma Dar es salaam Jumamosi (Oktoba 28) yalishuhudia Ibrahim Class na Fadhili Majiha wakiibuka na ushindi dhidi ya mabindia kutoka China na Afrika Kusini.
Ibrahim Class Mgender Ibrahim Class alishinda ubingwa wa taifa uzani wa “Super Feather”, 58.9Kg kwa kumpiga bondia Xiao Tao Su wa China kwa majaji wote watatu kumpa ushindi Ibrahim Class baada ya mizunguko 10 ya pambano hilo kumalizika.
Fadhili Majiha Ubingwa wa WBC Afrika uzani uzani wa “Super Bantam” kwa mara ya kwanza tangu kutambulishwa kwake umepata bingwa wake wa kwanza, kwa kumshinda Bongani Mahlangu (Afrika ya Kusini) kwa point za majaji wote watatu baada ya kumalizika kwa mizunguko 10 ya pambano hilo.
Mapambano hayo mawili yalifanyika katika ukumbi wa PTA, Sabasaba, Dar es salaam.
Pamoja na kuwapongeza mabondia hao, Kamisheni pia inampongeza muandaaji wa pambano hilo Hb Sadc Boxig Promotion.
Naye Bondia Pius Mpenda ameshinda pambano lake dhidi ya Dauren Yeleussinov (Kazakhstan) katika pambano la mizunguko 10 lililofanyika tarehe 29 Oktoba, 2023 lililofanyika Istanbul, Uturuki. Pambano hilo lilikuwa la ubingwa “WBC Peace” pia na kufanya kuwa bingwa wa kwanza kutoka Tanzania kushinda ubigwa huo.