Katika utekelezaji wa kampeni ya “Ongea Nao” Mtandao wa Polisi Wanawake – TPF- Net, Mkoa wa Kipolisi Temeke umeanza utekelezaji kwa kuifikia Shule ya Sekondari Kibasila iliyopo Manispaa ya Temeke na kuongea na Wanafunzi wa kidato cha kwanza.

Staff Sajent, Justine, Koplo Saumu, Konstebo Zainab na Betilda waliwasilisha elimu ya ukatili wa kijinsia, madhara ya ukatili, namna ya kujiepusha na ukatili, kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu, kuzidisha bidii katika masomo yao na kumtanguliza Mungu, ili kujijenga zaidi katika imani zao.

Aidha, wanafunzi hao pia walielekezwa namna ambavyo kampeni ya ”Ongea nao” imelenga kuwaokoa vijana na makundi mbalimbali ya jamii katika vitendo viovu ili kujijengea mustakabali mzuri wa maisha yao na kuelekezwa namna kampeni hiyo ilivyodhamiria kuibua vipaji vya vijana kupitia michezo na sanaa.

Wakipokea elimu hiyo, Wanafunzi waliimba nyimbo mbalimbali za uzalendo huku Walimu wa Shule hiyo wakiahidi kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuandaa michezo kwa Wanafunzi, ikiwemo mipira wa miguu na sanaa.

Nendeni mkasikilize kero za Wananchi - Dkt. Biteko
Umeme si anasa ni hitaji la lazima - Dkt. Biteko