Bodi ya Ligi Tanzania Bara ‘TPLB’ imeipiga kijembe Bodi ya Ligi nchini Misri, kufuatia ushindi wa Simba SC dhidi Al Ahly kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika uliochezwa jana Jumanne (Februari 23), Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es salaam.

TPLB imepiga kijembe hicho kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii (Facebook na Instagram), kwa kuutumia ushindi wa Simba SC kwenye mchezo huo, ambao ulifuatiliwa na mashabiki wengi katika ukanda wa Afrika mashariki na kati.

Mapema hii leo kurasa za mitandao ya kijamii za TPLB zimeonesha nembo ya Ligi Kuu Tanzania Bara ‘VPL’ kama mwakilishi wa Simba SC, huku nembo ya Ligi Kuu ya Misri ikiiwakilisha Al Ahly.

Kisha maelezo ya picha hiyo yanasomeka:

Full Time

Vodacom Premier League 1-0 Egyptian Premier League

#VPL

Bao la Simba SC kwenye mchezo huo lilifungwa na mshambuliaji kutoka nchini Msumbiji Luis Miquissone kipindi cha kwanza na kuibua shangwe kwa mashabiki na wanachama wa klabu hiyo.

Masau Bwire aipongeza Simba SC, 'MSIJISAHAU'
Kaze afichua siri nzito Young Africans