Chuo kikuu cha Dar es Salaam – UDSM, kimeingia mkataba wa makubaliano na Taasisi ya Sekta Binafsi TPSF, kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi Kiuchumi – HEET, ili kuwajengea uzoefu wahitimu wa vyuo vikuu nchini, wanapoingia kwenye ajira na kumudu changamoto mbalimbali.

Akizungumza mara baada ya zoezi la utiaji saini, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPSF, Raphael Maganga alizielezea takwimu za wanafunzi ambao hawana ajira na namna mradi huo utakavyo wasaidia zaidi ya wanafunzi 800,000 hadi milioni moja kila mwaka.

Amesema, “kati yao chini ya asilimia 15 wanaajiriwa kwenye ajira rasmi. Makubaliano haya kati ya UDSM na TPSF yanalenga kutatua changamoto hii kwa kuangalia ni jinsi gani Sekta Binafsi itaweza kuajiri wahitimu wengi na Vyuo kuwa na mitahala inayoenda na mahitaji na mabadiliko ya biashara” alisema Bw. Maganga.”

Kwa upande wake Mgeni rasmi, Katibu Mkuu wa wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo alisema mradi huo wa HEET, licha ya kuwa utasaidia kuongeza uzoefu kwa wahitimu pia utatumika katika maboresho ya mitaala ili iendane na mahitaji ya soko la ajira.

Naye Makamo wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, Prof. William Anangisye alielezea namna mradi wa HEET utakavyoendana na mahitaji ya soko la ajira nchini ili mikataba hiyo iweze kuwasaidia wahitimu kujiajiri na kwamba mikataba hiyo pia iweze kutoa ujuzi walionao kusaidia taasisi walizoingia nazo mkataba.

Mradi huo wa HEET, unafadhiliwa na benki ya dunia ukiwa na lengo kuu la kuboresha utoaji wa elimu ya juu, ili kuzalisha wahitimu wanaoendana na mahitaji ya soko.

Prince Dube bado yupo sana Azam FC
Maafande Ligi Kuu kuweka kambi Shinyanga, Zanzibar