Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF). Godfrey Simbeye amesema kuwa serikali inahitajika kuweka mazingira yatakayo changia kuwa na sera ambayo italenga kukuza haraka sekta ya wajasirimali ili kuongeza ajira, vipato vya wajasiriamali na pato la taifa na kupunguza umasikini katika jamii.

“Sera iliyopo ya mwaka 2003 ya kuendeleza ujasiriamali inahitaji kuboreshwa zaidi ili kwenda na wakati ili kukuza na kuimarisha maendeleo ya sekta hii” alisema. Simbeye.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Uwekezaji Prof. Adolf Mkenda amesema  kuwa sekta ya ujasiriamali ina mchango mkubwa kwa Taifa, na Serikali imekuwa karibu katika kuhakikisha inazidi kuimarika  na kutoa mchango mkubwa.

“Pamoja na mchango huu wa sekta hii pia tunatambua kuna changamoto mbalimbali ambazo kwa kushirikiana na wadau wa biashara tunaweza kuifanya sekta hii kuimarika zaidi na kuwa na mchango mkubwa kuliko ilivyo hivi sasa,” alisema Prof. Mkenda.

 

Video: Majaliwa ampa wiki moja Mwakyembe, ni kuhusu mkataba wa Mawakili Afrika Mashariki
Audio: JPM ajibu kero ya wananchi Ubungo kupitia simu ya Makonda 'live'