Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA imesema kuwa haina mpango wa kulumbana na Askofu Zakaria Kakobe bali inatekeleza maelekezo ya Kamishna Mkuu.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Elimu ya Mlipa Kodi wa Mamlaka hiyo, Richard Kayombo ambapo amesema kuwa maofisa wao wanaendelea kutekeleza agizo la Kamishna Mkuu wa TRA, Charles Kichere la kuchunguza utajiri wa Askofu huyo.

“Sisi TRA hatutaki kuwa kwenye malumbano na Askofu Kakobe, tulichosema tumeishia hapo, alichosema Kamishna Mkuu tutaishia hapo hapo, hatutakiwi kujibizana naye,”amesema Kayombo

Aidha, katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es salaam, Kamishna Mkuu, Charles Kichere alisema kuwa Mamlaka yake imepokea kwa furaha kauli ya Kakobe kuhusu utajiri wake na inataka kujirisha vyanzo vya utajiri wake.

Hata hivyo, Askofu Kakobe aliishauri TRA kutohangaika naye badala yake ikatafute fedha sehemu nyingine, huku akieleza kuwa ana nyumba moja tu iliyopo Kijitonyama jijini Dar es salaam.

Joseph Mbilinyi aitwa kituo cha polisi
Simba kufanya makubwa Mapinduzi Cup