Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Njombe imefanikiwa kukusanya bilioni 14.9 ya mapato katika mwaka wa fedha 2018/2019 hadi sasa, licha ya bajeti ya makadilio kuwa bil. 17 na kutoa pongezi kwa wilaya ya Njombe ambayo imekusanya zaidi ya asilimia 70.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa wiki ya elimu kwa mlipa kodi mkoani Njombe iliyofanyika mjini Makambako, Afisa mwandamizi wa kodi mkoani humo, Adeliki Alphonce amesema kuwa licha ya kufanikiwa kukusanya kiasi hicho cha fedha lakini bado kuna upungufu wa shilingi bilioni 3.1 ili kukamilisha lengo.

“Mpaka sasa wananchi wenzangu tumeweza kukusanya shilingi bilioni 14.9 katika yale malengo ya bilioni 17 bado tunaupungufu wa bilioni 3.1 kwa hiyo wafanyabiashara tujitoe katika muda uliobaki tuweze kufikisha lengo, tuzitumie hizi mashine za Elektroniki na tusione kama TRA wanakuja kutusumbua,”Amesema Alphonce

Aidha, katika kuhakikisha mkoa wa Njombe unakuwa kinara kwa ukusanyaji wa mapato, mkuu wa wilaya ya Njombe, Ruth Msafiri akizindua wiki ya elimu kwa mlipa kodi amezitaka halmashauri kuondoa vikwazo visivyo na tija kwa wawekezaji wa viwanda ili kuwavutia wawekezaji na kukuza uchumi wa kaya, mkoa na taifa kwa ujumla.

“Kama alivyotueleza mh.Rais alipokuwa kwenye mkutano wake wa kwanza katika mkoa wa Njombe kwenye wilaya ya Njombe sehemu inaitwa Lwangu halmashauri ya mji wa Njombe alisema, tunatabia ya kuchelewesha wawekezaji na haya yanafanywa ndani ya halmashauri na mimi nirudie kuwaomba wale wanaohusika na ardhi saidieni ili tuhakikishe kwamba ili tuweze kulipa kodi na kwa ziada na sisi mchango wetu uonekane mkubwa zaidi tupate viwanda”amesema Msafiri

Dkt. Mwigulu adai ushindi wa CCM hautokani na Wakurugenzi
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZA UANDISHI WA HABARI/UTANGAZAJI - DAR24 MEDIA