Mamlaka ya Mapato Tanzania – TRA, Mkoa wa Kikodi wa Kariakoo imebandika stika maalumu kwa ajili ya uzinduzi rasmi wa kuhamasisha wafanyabiashara kutoa risiti pale wanapouza bidhaa zao na wananchi kudai risiti, ambayo itakuwa thamani sawa na bidhaa waliyonunua kwa maendeleo ya Taifa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Meneja Msaidizi wa ukaguzi TRA Mkoa wa Kikodi Kariakoo, Thoddy Beyanga amesema kuwa kampeni hiyo itakuwa maalumu kwaajili ya kuhamasisha matumizi mazuri ya mashine za kieletroniki – EFD, kwa wafanyabiashara nchini.

Amesema, “unapouza toa risiti na vile vile unaponunua bidhaa udai risiti yako. Tumebaini kuporomoka kwa utoaji wa risiti kwa sababu risiti zinazotolewa zimekuwa tofauti na matarajio nayo inapelekea makusanyo kushuka.”

Beyanga amefafanua faida za kutoa na kudai risiti pale biashara inapofanyika kuwa inasaidia kutunza kumbukumbu katika ukadiliaji wa mapato yanayoendana na uhalisia wa biashara ambayo mfanyabiashara amefanya pamoja na kuchangia pato la taifa.

Kwa Upande wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Boss Shopping Centre, Hanif Janmohamed amesema kuwa amejisikia vizuri kwa TRA kuendelea kuhamasisha wafanyabiashara kulipa kodi kwa kutoa risiti halali kulingana na bidhaa iliyonunua.

Pia ametoa wito kwa wafanyabiashara kulipa kodi kwa maendeleo ya nchi pia amesema kuwa kutoa na kudai risiti ni wajibu wa kila mmoja kwa maendeleo ya nchi, huku TRA ikidai kuwa kampeni ya uhamasishaji wa wafanyabiashara kutoa risiti na wananchi kudai risiti ni endelevu, hivyo jamii inatakiwa kutekeleza bila shuruti.

Wataalam, Mawaziri wa Afya wapanga kuyakabili magonjwa
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Agosti 29, 2023