Mamlaka ya Mapato Tanzania – TRA, leo Novemba 8, 20223 imeanza Wiki ya shukrani kwa mlipakodi ambapo itatambua walipakodi wao waliofanya vizuri katika mwaka wa fedha wa 2022/23.

Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipakodi na Mawasiliano, Richard Kayombo amesema kilele cha wiki hiyo ni Novemba 24, 2023 na kitafanyika jijini Dar es Salaam, mgeni rasmi akiwa Naibu Waziri Mkuu, Dotto Biteko ambapo shindano la vilabu vya kodi kwa shule za Sekondari za Dar es Salaam na Pwani ambapo shule 59 zitashiriki.

Mkurugenzi wa Elimu kwa mlipa kodi na mawasilano TRA, Richard Kayombo akizungumza na waandishi wa Habari makao makuu ya ofisi zao jijini Dar es Salaam leo Novemba 8, 2023 kuhusu wiki maalum ya kuwashukuru na kuwapongeza walipa kodi kwa hiari na wakati itakayoanza Tar 18 hadi 24 siku ya kilele chake.

Amesema, “hawa ni wale walipakodi waliotoa ushirikiano kwa maofisa wetu ikiwemo kutoa taarifa za ukaguzi na hata ritani pale walipohitajika ambao waliotekeleza sheria ya kodi, lengo ni kuhakikisha wanajenga uhiyari wa kulipa kodi kwa vijana wadogo ili wanapokuwa watu wazima wawe walipakodi wazuri.”

Kayombo amesema Vijana hao wanapaswa kufahamu umuhimu wa kulipa kodi kwani wapo watakaokuwa Wafanyabiashara, Wakandarasi na Wafanyakazi ndani ya TRA na kwamba mwaka wa fedha uliopita, makundi mbalimbali yalipata tuzo hizo na mshindi wa jumla alitoka kwenye sekta ya fedha.

Aidha, amesema kwa mwaka huu wanaamini watu wengi wanazidi kuhamasika, ili waweze kutambulika kwa kazi nzuri ya kulipa kodi, ambapo kaulimbiu ni ‘Kodi yetu, maendeleo yetu, tuwajibike ikilenga watu walipe kodi, wadai risiti wafanyapo manunuzi na kutoa taarifa ya wanaokwepa kodi.’

Mamlaka ya Mapato – TRA, hutumia wiki hiyo kuwatambua wale waliolipa kodi kwa hiari na wale waliotoa ushirikiano wa kutosha kulipa kodi lengo ni kuwatia hamasa walipakodi wote waliolipa kodi zao kwa hiari, bila kusukumwa wala kufuatwa fuatwa.

Casemiro: Ninajuta kusajiliwa Manchester United
Kocha Singida FG akiri mambo magumu