Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) imetoa ufafanuzi kuhusu tangazo kwa watumishi wake linalowataka kutangaza mali na madeni yao lililotolewa na Kaimu Kamishina Mkuu wa Mamlaka hiyo, Dk. Philip Mpango.

Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipa Kodi (TRA), Richard Kayombo aliwaambia waandishi wa habari kuwa tangazo hilo kwa watumishi wake lililenga katika kupata taarifa hizo kwa ajili ya matumizi ya kiofisi (ndani) na sio kwa ajili ya kuyaweka hadharani kwa umma.

“Hayo ni mambo ya ndani ya TRA, hatubanwi kisheria kutangaza mali na madeni ya watumishi wetu. Taarifa hizo ni kwa ajili ya matumizi ya ndani ya kiutawala,” alimwambia mwandishi wa The Citizen.

Katika hatua nyingine, Kayombo alieleza kuwa taratibu za kuchukua hatua za kisheria dhidi ya makampuni 15 yaliyokwepa kodi bandarini zinaendelea kuchukuliwa.

Afisa Wa Jeshi la Polisi Ajinyonga
Chadema wapaza sauti za Kilio Chao Kwa rais Magufuli