Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imelishukia Baraza Kuu la Waislamu Tanzania kutokana na kuwepo ongezeko kubwa la maombi ya misamaha ya kodi.

TRA imeiandikia Barua Bakwata baada ya kubaini kuwa kati ya mwaka 2006 na Septemba mwaka huu, Baraza hilo limeingiza magari 82 yenye msahama wa kodi.

Kwa mujibu wa Mtanzania, barua hiyo ya TRA kwenda Bakwata ilisainiwa na Meneja Misamaha ya Kodi wa TRA, Mwamtum Salim inamueleza Katibu Mkuu wa Bakwata kuwa kutokana na kuwepo ongezeko kubwa la maombi ya misamaha ya Kodi, Mamlaka hiyo itaanza kufuatilia kwa ukaribu zaidi maombi hayo.

TRA ilitoa siku saba kwa Baraza hilo kuhakikisha inawasilisha nyaraka kadhaa ikiwa ni pamoja kuonesha safari za magari, bima, stakabadhi ya mafuta, uthibitisho kuonesha fedha zilizonunua magari hayo pamoja na kitabu cha mahesabu cha Taasisi hiyo.

Mwenyekiti Wa UWT (CCM) Ahamia Chadema
Kimbunga Cha Magufuli Chafyeka Maafisa Tanesco