Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) imewataka wananchi kuendeleza utaratibu wa kulipa kodi mbalimbali kwa wakati huu ambao mamlaka hiyo inaendelea na utaratibu wa kuanzisha vituo vipya vya huduma za kikodi kwa mlipa kodi.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Elimu kwa mlipakodi Richard Kayombo mara baada ya kutembelea kituo kipya cha huduma za kikodi kilichoanzishwa eneo la Chanika jijini Dar es salaam.

Amesema kuwa kwa sasa huduma mbalimbali zitapatikana hapo huu ukiwa ni mikakati wa Mamlaka hiyo kusogeza huduma karibu zaidi kwa wananchi.

“Kuanzishwa kwa kituo hiki cha huduma za kikodi hapa Chanika itawasaidia wafanyabiashara wengi kupata huduma kirahisi zaidi tofauti na umbali mrefu uliokuwa ukiwakabili, TRA ni yenu msisite kuzitembelea ofisi hizi na kuuliza huduma yoyote,” amesema Richard Kayombo.

Lori la mafuta lalipuka na kuua 23 katikati ya mji
Putin aivuruga CIA Marekani, 'anamsaidia Trump kushinda kijanja'

Comments

comments