Mamlaka ya Mapato Tanzannia (TRA) imetangaza mpango wa kuanza kukusanya kodi kwenye nyumba za kupangisha ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kupata fedha ambazo Serikali ilikuwa haipati kutoka kwenye vyanzo vyake.

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo aliwaambia waandsihi wa habari jana jijini Dar es Salaam kuwa Mamkala hiyo itafanya uhakiki wa nyumba za kupanga na kubaini gharama za kodi.

Aliwataka wananchi wanaopanga katika nyumba hizo kuhakikisha wanashirikiana na TRA kueleza bei ya nyumba na kuepuka kufanya udanganyifu ili wasikumbwe na mkono wa sheria.

“Natoa wito kwa wapangaji na wapangishaji kujiepusha na aina yoyote ya udanganyifu katika suala zima la kodi halisi ya pango kwa kuwa inaweza kuwasababishia kushtakiwa endapo udanganyifu huo utabainika,” alisema Kayombo.

Kayombo alieleza kuwa lengo la Mamlaka hiyo ni kuhakikisha Serikali inapata kodi yote ambayo imekuwa ikikosa kutoka kwa vyanzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na nyumba.

Kayombo alieleza kuwa mwezi Julai, Mamlaka hiyo ilikusanya kiasi cha shilingi trilioni 1.055 ambazo ni sawa na asilimia 95.6 ya lengo walilopangiwa na Serikali kwa mwezi huo, ambazo ni shilingi trilioni 1.103.

Polisi wajipanga kumzuia Lissu kutumia mitandao ya kijamii
Mwakyembe atetea Serikali kukata rufaa ndoa za utotoni