Mamlaka ya Mapato nchini – TRA, imewapa Wakulima misamaha ya kodi katika uagizaji wa Trekta, Kitalu nyumba, Mbolea na pembejeo za Kilimo.
Hayo yamebainishwa na Ofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania – TRA, Mkoa wa Mbeya, Nicodemas Massawe katika maonesho ya nanenane yanayondelea Viwanja vya John Mwakangale Mkoani Mbeya.
Amesema, “Mkulima anayepaswa kulipa kodi ni yule ambaye kwa mwaka thamani yakeinafikia shilingi milioni nne na kuendelea, lakini chini ya hapo anasamehewa, watembelee banda letu ili wajue ni vitu gani vimesamehewa kodi.”
Hata hivyo, Massawe amebainisha kuwa “sheria yetu ya kodi ya mapato imeweka utaratibu kuwa chama chochote cha ushirika ambacho mapato ghafi yake hayazidi milioni 100 kwa mwaka nacho kimesamehewa kodi.”