Baaadhi ya Wananchi wameoneshwa kufurahishwa na taarifa zilizotolewa juu ya kuanza kwa huduma ya Treni ya SGR (Mwendokasi) na kusema hatua hiyo ni mwanzo wa mafanikio katika maendeleo ya Taifa huku wakisema itasaidia kuharakisha shughuli za kimaendeleo.

Wakiongea kwa nyakati tofauti, Wananchi hao akiwemo Hamisi Simwesa ambaye amesema ana tumai kuwa ahadi za kuanza safari hii itakamilika kutokana na mara kadhaa kutolewa bila mafanikio na hivyo kuwakatisha tamaa Wananchi.

Amesema, “Ahadi zimekua nyingi kuliko safari yenyewe, tatizo wenye mamlaka nchi hii Huwa wanajisahau walichowahi kiahidi na kidhani wanao waambia ni watoto wasio na uelewa, lakini nampongeza Kadogosa (Mkurugenzi Mtendaji – TRC) amepiga hatua.

Ujenzi wa Relei ya Mwendokasi – SGR.

Naye, Himid Liwidu, amesema “mimi nilishaga kata tamaa kuhusu hiyo tuleni (Treni) ya umeme lakini naamini kwasasa hali itakuwa tofauti na tutaiona kweli katika muda uliopangwa ikianza safari zake na hapo nitakuwa na lakuongeza ila kwasasa tusubiri.”

Machi 22, 2023, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania – TRC, Masanja Kadogosa Kadogosa akiwa Jijini Dodoma alisema Treni ya Mwendokasi inatarajia kuanza safari kwa kipande kilichokamilika mwishoni mwa mwezi April au mwazoni mwa mwezi MEI 2023.

Hatua hii inakuja ikiwa ni muda mchache baada ya Wajumbe wa Baraza Kuu la Wanawake wa CCM kutumia usafiri wa Treni ya Mkandarasi kutokea Dar es salaam hadi Dodoma, ili kushuhudia mwenendo wa ujenzi wa Reli ya kisasa -SGR.

Watakiwa kuimarisha mifumo manunuzi ya bidhaa za Afya
Utalii: Nchi 10 zilizotembelewa zaidi Duniani