Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda amesema Serikali ya Awamu ya sita ya Rais Samia Suluhu Hassan imetoa kipaumbele kwa sekta ya elimu ambapo imeweka msukumo katika kuongeza bajeti.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Machi 9, 2022 Waziri Mkenda amesema kupitia fedha za UVIKO 19 shilingi Trioni 1.3 robo ya fedha hizo zimewekezwa katika sekta hiyo ambazo zimewezesha ujenzi wa miundombinu ya elimu katika ngazi zote pamoja na kununua vifaa vya kufundishia na kujifunzia.

Amesema kuwa bajeti ijayo watahakikisha inawaangalia wanafunzi wa kidato Cha sita waliofanya vizuri zaidi masomo ya sayansi na kuwapeleka nje ya nchi katika vyuo Bora zaidi.

Amesema lengo la Mhe. Rais ni kuhakikisha kila mtoto wa kitanzania anapata fursa ya masomo bila changamoto zozote na ndio maana ameagiza wanafunzi wote waliokatisha masomo kwa sababu yeyote warudi shuleni

Kuweka akiba husaidia utulivu wa akili
Habari picha: Rais Samia akutana na wake wa viongozi