Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) utakamilika kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa, ili uweze kuleta tija kwa Watanzania.

Akizungumza Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba wa ujenzi wa reli hiyo awamu ya tatu kipande cha kutoka Makutupora hadi Tabora, Rais Samia amesema Serikali imewekeza takribani shilingi trilioni 14 .7 kwenye mradi huo, hivyo ni lazima uwe ni wenye maslahi kwa Taifa.

Rais Samia ametumia hafla hiyo kusisitiza kuwa miradi yote mikubwa inayotekelezwa na Serikali itakamilika kwa wakati uliopangwa, ili Wananchi waweze kunufaika.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania, Masanja Kadogosa amesema ujenzi wa SGR awamu ya tatu kipande cha kutoka Makutupora hadi Tabora utagharimu zaidi ya shilingi trilioni 4.4 na ujenzi wake utakuwa wa muda wa miezi 46.

Mradi wa Reli ya kisasa awamu ya tatu kipande cha kutoka Makutupora hadi Tabora kina urefu wa kilomita 368.

Waziri Aweso afanya mabadiliko haya
Maiti 200 zafukuliwa Dar es Salaam