Rais wa Marekani,  Donald Trump amewasili nchini Korea ya Kusini kwa ziara ya kikazi ya mashariki mwa bara la Asia.

Katika mtandao wake wa Twitter, Rais Trump amemuelezea Rais wa Korea Kusini, Moon Jae-in kuwa ni mtu mwema na kuongeza kuwa watafanya kazi kwa pamoja kuweza kushughulikia kitisho cha nyuklia kutoka Korea kaskazini.

Hata hivyo, Rais Trump amesema kuwa mbinu ya Rais huyo wa Korea Kusini ambayo ni mbinu shirikishi dhidi ya Korea ya Kaskazini kama ya makubaliano na kwamba raia wa Korea Kusini walikuwa na wasiwasi na kauli za mabavu za Rais Trump kwamba zinaweza kuifanya Korea ya Kaskazini kuchukua hatua za kijeshi katika eneo hilo.

 

Waliokosa mikopo watakiwa kukata rufaa
Makamu wa Rais wa Zimbabwe afutwa kazi