Maafisa wa Shirika la Upelelezi la Marekani, FBI wamezipekua ofisi za wakili binafsi wa Rais wa Marekani, Donald Trump, Michael Cohen. kitendo ambacho Trump amelikosoa vikali shirika hilo.
Wakili wa Cohen, Stephen Ryan amesema kuwa upekuzi huo uliofanyika ni sehemu ya maelekezo kutoka kwa, Robert Mueller mwanasheria anayeoongoza uchunguzi kuhusu ushirikiano kati ya timu ya kampeni ya Rais Trump pamoja na Urusi wakati wa uchaguzi wa urais uliofanyika mwaka 2016.
“Nimesikia kwamba wamevamia ofisi ya mmoja wa mawakili wangu binafsi, hali hii ni ya aibu. hili ni shambulizi dhidi ya nchi yetu, kwa maana halisi. ni shambulizi katika kile ambacho sisi wote tunakisimamia, walichokifanya si sahihi hata kidogo,”amesema Trump
Hata hivyo, Gazeti la The New York Times limeripoti kuwa uvamizi huo hauhusiani na maelekezo ya Mueller kuhusu uchunguzi katika ofisi hizo.
-
Spika ajiuzulu kukwepa kura ya kung’olewa
-
Kesi ya kuondolewa ukomo wa umri wa urais Uganda ‘yawaka’
-
Marekani kuchukua maamuzi magumu dhidi ya Syria