Rais wa Marekani Donald Trump, ameendelea kuwashambulia waandishi wa habari kwa kuwakejeli na kuwalingishia barua aliyoandikiwa na rais mstaafu wa nchi hiyo Barack Obama, akiwaambia licha ya kiu ya habari waliyokuwa nayo, hatafichua ujumbe uliomo kwenye barua hiyo.
Kwa kawaida nchini Marekani, rais anayeondoka madarakani humuandikia ujumbe wa barua rais mpya, ujumbe ambao hubeba mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ushauri unaozingatia uzoefu wa mhusika katika Ikulu ya nchi hiyo.
“Nilipofika tu ofisini nikaikuta barua hii iliyoandikwa kwa umahiri mkubwa kutoka kwa rais mstaafu Obama, Ni uungwana wa hali ya juu kwake kuniandikia barua hii, kwa kweli tunaenzi ujumbe wake. Tutaufanyia kazi ujumbe huo na vile vile hatuwezi kufichua ujumbe husika kwenu waandishi wa habari,”amesema Trump.
Trump amegoma kutoa taarifa ya ujumbe ulioandikwa na rais mstaafu Barack Obama, kwenye barua hiyo kitu ambacho si kawaida ya marais wa Marekani kufanya hivyo mbele wa waandishi wa habari.