Rais wa Marekani Donald Trump amekataa kuidhinisha matumizi ya karibu dola Billioni 900 zilizopitishwa na Bunge na Baraza la Wawakilishi ili kusaidia familia na makampuni yaliyoathiriwa na Corona nchini humo.
Mpango huo uliopigiwa kura kwa wingi katika taasisi zote mbili kwa wingi na kukataliwa na maseneta saba ungewezesha familia nyingi kupokea hundi ya dola 600 mapema wiki ijayo, kama alivyoahidi Waziri wa fedha Steven Mnuchin.
Rais Trump anataka sheria iliyorekebishwa ambayo itamuwezesha kila mtu mzima apokee dola 2000 na sio dola 600.
Sheria iliyokataliwa na Trump ilikuwa inatoa dola Bilioni 900 kusaidia familia na wafanyabiashara walio katika matatizo na dola Bilioni 1.4 kufadhili matumizi ya serikali.