Rais wa Marekani, Donald Trump amesema kuwa amekatishwa tamaa na China kufuatia ripoti iliyotolewa kuwa inasafirisha mafuta kwenda Korea Kaskazini.

Katika Ujumbe wake wa twitter, Rais Trump amesema kuwa China imeonekana hadharani ikiruhusu mafuta hayo kwenda Korea Kaskazini.

Wiki iliyopita, China iliunga mkono azimio la Umoja wa Mataifa lililoandikwa na Marekani ambalo lilishirikisha hatua za kupunguza kiwango cha mafuta kinacheolekea Korea Kaskazini kwa asilimia 90.

”Tunatoa wito kwa China kusitisha uhusiano wowote wa kiuchumi na Jamhuri ya kidemokrasi ya Korea Kaskazini ikiwemo utalii pamoja na uuzaji wa mafuta ama bidhaa za mafuta na chochote kile,” amesema Michael Cavey msemaji wa Ikulu ya Marekani.

Hata hivyo, matamshi hayo ya rais Trump dhidi ya China yamekuja mara baada ya gazeti moja la Korea Kusini Chosun IIbo kuripoti kuwa meli za China zimekuwa zikisafirisha mafuta kwa siri kupitia baharini kuelekea Korea Kaskazini.

 

Mahakama kuu: Bunge lilishindwa kumshughulikia Zuma
Magazeti ya Tanzania leo Desemba 30, 2017