Kamati ya Bunge la Marekani inayochunguza matukio yaliyopelekea shambulizi la Bunge la Januari 6, mwaka 2021, limepiga kura kwa kauli moja jana Alhamisi, na kumtaka Rais wa zamani Donald Trump, kuitwa ili kutoa ushuhuda wake.
Jopo la wabunge hao, limeonyesha pia video mpya inayozua utata ambayo inawaonyesha wasaidizi wa karibu wa Trump, wakielezea mpango wake madhubuti, wa kutengua matokeo ya uchaguzi ya mwaka 2020.
Wachambuzi wanasema, matamshi ya Trump ndiyo yalipelekea wafuasi wake kutekeleza shambulizi baya dhidi ya bunge la Marekani ambapo hata hivyo Trump mwenyewe amekosoa na kuipinga ripoti ya kamati hiyo.
Kamati hiyo, ilitumia zaidi ya saa mbili kufikia maamuzi hayo ikipitia taarifa kutoka kwa wanachama, nyaraka, na ushahidi uliorekodiwa kwamba Trump pia alishindwa kuwaondoa maelfu ya wafuasi waliovamia Capitol na kwamba madai yake yalikuwa ni uwongo na aliiba kura hata kama washauri wake wa karibu walimwambia kuwa ameshindwa.
Hata hivyo, Kamati hiyo teule ya Bunge imekuwa ikichunguza shambulio hilo la Ikulu, ambalo lilisababisha zaidi ya maafisa wa polisi 140 kujeruhiwa na vifo vya watu kadhaa kwa zaidi ya mwaka mmoja, huku zaidi ya mashahidi 1000 wakiwahoji.
Awali, Mawakili wa Trump waliiambia Mahakama ya Juu kwamba Dearie anapaswa kuwa na uwezo wa kuhakiki rekodi hizo na kwamba Idara ya Haki “imejaribu kuhalalisha mzozo wa usimamizi wa hati na sasa inapinga vikali mchakato wa uwazi ambao hutoa uangalizi unaohitajika.”