Rais wa Marekani Donald Trump anakabiliwa na tuhuma kuhusiana na kauli aliyoitoa kwa mjane wa mwanajeshi wa nchi hiyo aliyeuawa vitani nchini Niger, ambapo inasemekana kuwa Trump alimwambia mjane huyo mumewe ambaye ni mwanajeshi alikuwa anajua kile alichokisaini kwa kazi anayojua hatma yake.

Kufuatiwa kauli hiyo Rais Donald Trump amekana kuhusishwa na kauli hiyo na kusema kuwa tuhuma hiyo ni ya kutungwa na haina ukweli ndani yake.

Mama mzazi wa mwanajeshi aliyeuawa ameunga mkono tuhuma aliyotuhumiwa Trump na kusema kuwa Rais huyo hakuwa na huruma wakati anawasiliana  na mke wa marehemu.

Mama mzazi wa mareheme amesema “Rais Trump hakumuheshimu mwanangu na mkewe pamoja name na mume wangu” Cowanda Jones-Johnson.

Mbunge Federica Wilson amesema kuwa alimwambia Myeshia Johnson: Alijua alichokuwa ametia Saini, ”lakini nadhani ni uchungu bila shaka”.

Sajenti La David Johnson amekuwa mmoja wa wanajeshi maalumu waliouawa baada ya kuvamiwa na wapiganaji wa kiislamu nchini Niger mwezi huu.

 

 

Rabah Madjer abebeshwa zigo AFCON 2019
Video: Mwigamba abwaga manyanga ACT- Wazalendo