Siku chache, baada ya nyumba Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump kufanyiwa uchunguzi na F.B.I. kiongozi huyo sasa amegomea suala la kuapa kabla ya kuhojiwa na wanasheria mkuu wa Jimbo la New York, Letitia James.
Rais huyo wa zamani, alitakiwa kula kiapo hiko kabla ya kujibu kila swali lililoulizwa na wachunguzi wake kwa kurudia maneno “jibu sawa” na kisha kuendelea na mahojiano dhidi ya shutuma zinazomkabili ikiwemo kushindwa kuitoa ushirikiano kwa maafisa wa upelelezi.
Trump, kwa kiasi kikubwa anaweza kuamua hatma ya mwenendo wa kesi yake ya madai mbalimbali yanayomkabili, ili kujua ikiwa rais huyo wa zamani alipandisha thamani ya mali yake kwa njia ya ulaghai na kupata mikopo na marupurupu mengine.
Kwa muda mrefu, amekuwa akipuuza madai hayo kiasi cha kukwamisha uchunguzi husika, lakini alilazimika kuketi na kuhojiwa chini ya kiapo baada ya majaji wengi kutoa uamuzi dhidi yake msimu huu.
Baadhi ya watu wenye ufahamu wa shauri hilo walisema, “yalikuwa ni shambulio la wazi dhidi ya mwanasheria mkuu na uchunguzi wake.”
Amesema, “Huu ni muendelezo wa wawindaji wakubwa zaidi wa wachawi katika historia ya nchi yetu.” na kubainisha kuwa analengwa na mawakili, waendesha mashtaka na vyombo vya habari.