Rais wa Marekani Donald Trump amemfukuza kazi Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo, Rex Tillerson na kumteua mkuu wa Shirika la Kijasusi, CIA, Mike Pompeo kuziba nafasi hiyo.
Trump amesema kuwa amefikia hatua ya kumfukuza kazi waziri huyo ili kuimarisha timu yake ya mawaziri kabla ya kuanza mazungumzo na Korea Kaskazini na baadhi ya mikutano mengine ya kibiashara.
Aidha, Tillerson alikuwa kwenye ziara rasmi ya Afrika wiki iliyopita wakati ambapo alipata taarifa za ghafla za Trump kukutana na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un.
Katika ziara yake alitarajiwa kuzitembelea Chad, Djibouti, Ethiopia, Nigeria na Kenya ikiwa ni ziara yake ya kwanza barani Afrika.
Hata hivyo, Siku ya Jumamosi ,msemaji wake alisema amesitisha shughuli alizokuwa anapaswa kufanya nchini Kenya kutokana na hali yake ya kiafya kutokuwa nzuri.