Rais wa Marekani Donald Trump amesema amemfuta kazi Mkuu wa Usalama wa Mtandao na Shirika la Usalama wa Miundombinu ya Uchaguzi (CISA), Chris Krebs kwa kile alichodai kuwa “taarifa zake zisizo sahihi kwa kiwango cha juu kuhusu maadili ya kura”.

Trump amekataa kukubali kushindwa katika uchaguzi wa Marekani, akitoa madai yasiyo na ushahidi ya wizi wa kura ingawa Maafisa wa Uchaguzi wanasema uchaguzi wa mwaka huu ulikuwa moja ya chaguzi salama zaidi  katika historia ya Marekani.

Wiki iliyopita Rais Trump alimfuta kazi Waziri wa Ulinzi, Mark Esper, huku kukiwa na ripoti kwamba alikuwa na wasiwasi juu ya utiifu wa mkuu huyo wa Pentagon.

Kumekuwa na tetesi mjini Washington DC kwamba kabla ya Trump kuondoka madarakani mwezi Januari, Mkuu wa CIA, Gina Haspel na mkurugeni wa FBI Christopher Wray huenda wakawa miongoni mwa wale watakaofutwa kazi na Trump.

Mirerani, mgodi wenye ulinzi zaidi Tanzania
Muswada wa kutomshtaki Rais umeungwa mkono na Bunge la Urusi