Rais wa Marekani, Donald Trump ametoa msamaha kwa wafungwa zaidi ya 140 miongoni mwao akiwa ni rapa Lil Wayne huku rapa mwingine Kodak Black na aliyekuwa meya wa Detroit, Kwame Kilpatrick, wakipunguziwa vifungo vyao.

Msamaha huo ambao unawadia saa kadhaa kabla ya kuapishwa kwa Rais mteule Joe Biden, pia umemjumuisha aliyekuwa mshauri wake Steve Bannon, ambaye anakabiliwa na mashitaka ya udanganyifu.

Bannon, ambaye alikuwa mshauri mkuu wa Rais Trump wakati wa kampeni yake mwaka 2016, alipatikana na hatia mwaka jana kwa makosa ya udanganyifu juu ya kampeni ya kuchangisha pesa kuhusiana na kujenga ukuta katika mpaka wa Marekani na Mexico.

Waendesha mashtaka, Bannon na wengine watatu,  walidanganya mamia ya maelfu ya wafadhili kuhusiana na mradi wa kampeni ya “Tujenge Ukuta ambayo ilikusanya dola milioni 25.

Hata hivyo, inadaiwa kuwa Bannon alipokea zaidi ya dola milioni 1 ambazo baadhi yake alizitumia kwa matumizi yake binafsi.

Taarifa kutoka Ikulu ya Marekani imesema kuwa kwa ujumla watu 73 wamepewa msahamaha huku wengine 70 wakipunguziwa vifungo vyao.

Bigirimana kuikosa Clube Desportivo 1º de Agosto
Dudu baya mikononi mwa sheria