Rais wa Marekani Donald Trump, amerejea tena kwenye kampeni za uchaguzi mkuu, kwa kufanya mkutano wa kwanza katika jimbo la Florida siku kadhaa baada ya kukutwa na maambukizi ya virusi vya Corona.

Akiwahutubia wafuasi wake huko Sanford, Florida, Trump amesema afya yake imeimarika na yuko huru kukutana tena na wapiga kura bila ya kuwa na wasiwasi wowote.

Trump anayewania muhula wa pili wa uongozi katika uchaguzi wa Novemba 3 nchini Marekani, alilazimika kukatiza kampeni yake kwa karibu siku 10 kufuatia kuambukizwa virusi vya Corona mnamo Oktoba 2.

Aidha Daktari wake amesema afya ya Rais Trump imeimarika, na kipimo alichofanyiwa hivi karibuni kimeonyesha hana tena maambukizi ya virusi vya corona na anaruhusiwa kusafiri.

Mkutano wa kampeni mjini Florida, jimbo ambalo ni muhimu kwa Trump kushinda, unafungua njia ya mikutano zaidi iliyopangwa kufanyika wiki hii katika majimbo ya Pennsylvania, Iowa na North Carolina.

Kocha Mwadui FC awaita Azam FC
Eneo la Mita 3500 Mlima Kilimanjaro kuharibiwa na moto