Mgombea wa Urais wa chama cha Republican Donald Trump ameulaumu utawala wa Bi Hillary Clinton wakati alipokuwa Waziri wa mambo ya nje kushindwa kudhibiti hali hali ya majanga yaliyotokea  nchini Iraq, Syria na Libya.

hillary-clinton-donald-trump

Trump ameyasema hayo wakati alipohutubia mkutano mkuu wa chama hicho ambapo alikubali rasmi uteuzi wa chama hicho kuwania kiti cha urais katika uchaguzi mkuu wa Novemba mwaka huu.

Trump amejielezea kama kiongozi mkombozi na sauti ya watu wanyonge  nchini Marekani huku akijitaja kama mtu mwenye sifa tofauti na mpinzani wake wa chama cha Democratic Hillary Clinton ambaye amemtaja kama kiongozi fisadi na asiyewajibika.

Katika mkutano huo Trump amesema taifa hilo haliwezi kufikia maendeleo ikiwa hakutakuwepo na utawala wa sheria thabiti huku akisema kuwa atawashughulikia raia wa nchi hiyo ambao wamesahaulika na kuongeza kwa kumtaja Bi. Hillary Clinton ambaye ni mpinzani wake kama Kiongozi fisadi

Aidha ameahidi kuwa atakabiliana na suala la wahamiaji haramu, akionya kuwa kwa sasa maelfu ya wahamiaji wameruhusiwa kuingia marekani bila kujali usalama wa taifa.

Katika Mkutano huo binti wa Tump ‘Ivanka Trup’ alimtaja babake kama kiongozi anayefaa kuongoza taifa hilo na kuwa atawajali wamarekani na kuwatetea.

JESHI LA POLISI KANDA MAALUMU YA DAR ES SALAAM LAKAMATA WATUHUMIWA SUGU
Picha 5 kutoka Mkutano wa Halmashauri Kuu ya taifa ya CCM Dodoma