Aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump anarajia kuanzisha mtandao wake wa kijamii katika siku za karibuni.
Baada ya kufungiwa katika mitandao ya kijamii kwa madai ya kuchochea uvunjifu wa amani Januari 6, Trump sasa amepanga kufungua mtandao wake mwenyewe.
Msemaji wa Trump wakati wa Kampeni za mwaka 2020, Jason Miller ameuambia mtandao wa Fox News kuwa ujio wa Trump kwa mtandao wake mwenyewe unatarajiwa ‘kubadilisha upepo.’
Hakuna taarifa zaidi zilizothibitishwa kutoka kwa Rais Trump, lakini mtandao huo unatarajiwa ndani ya kipindi cha miezi miwili au mitatu ijayo.