Rais wa Marekani amewaambia maelfu ya wafuai wake kuwa aliwaambia maafisa wa Marekani kupunguza kasi ya upimaji wa virusi vya corona (covid-19), kwa sababu idadi ya visa ilikuwa inapaa kwa kasi.
Akizungumza na wafuasi wake katika eneo la Tulsa, Oklahoma wikendi iliyopita, Rais wa Marekani ambaye anaitaja corona kwa jina la utani la ‘kung flu’ ambalo linatokana na kuitupia lawama China kuwa ndio chanzo, alisema kuwa upimaji wa virusi vya corona ni kama upanga mkali unaokata sehemu mbili.
“Unapopima watu wengi zaidi, unapata visa vingi zaidi. Kwahiyo, niliwaambia watu wangu wapunguze kidogo kasi ya upimaji,” alisema Rais Trump.
Hata hivyo, saa chache baadaye, Ikulu ya Marekani iliiambia Reuters kuwa alichokisema Trump kilikuwa sehemu ya utani tu.
Marekani imeshapima watu milioni 25 hadi sasa, ikiwa ni zaidi ya nchi nyingine zote. Zaidi ya watu 119,654 wamethibitika kupoteza maisha kutokana na virusi vya corona nchini Marekani, idadi ambayo inaifanya kuwa nchi inayoongoza kwa vifo vya corona ikifuatiwa na Brazil yenye vifo zaidi ya 50,000.
Rais Magufuli ataja sababu za kumuondoa Gambo na viongozi wengine Arusha