Rais wa Marekani, Donald Trump amependekeza adhabu ya kifo kwa watu watakaokutwa na hatia ya kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.
Trump ameyasema hayo katika hotuba yake ya New Hamphshire ambapo ameeleza kuwa kwa kutoa adhabu kali na kujiimarisha kiakili kama taifa, tatizo hilo linalotafuna nguvu kazi litakoma.
Ameonesha kutoridhishwa na adhabu za kifungo cha muda ambacho wanapewa watu wanaokutwa na hatia ya kujihusisha na dawa za kulevya huku wakiwa wamewasababishia matatizo makubwa na hata kifo watumiaji wa dawa hizo.
Amesema kuwa kutokana na kuliwekea kipaumbele suala hilo, Bunge limetenga kiasi cha dola bilioni sita katika bajeti mpya ya mwaka wa fedha 2018/19, kiasi ambacho amesema hakijawahi kutengwa katika masuala ya kupambana na dawa za kulevya.
“Kwanza kabisa tunapunguza kiwango uhitaji wa dawa hizo,kuhakikisha tunapunguza idadi ya watu wanaojiingiza na hatimaye kutekwa na matumizi ya dawa za kulevya,ni muhimu sana,” alisema.
- Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Machi 20, 2018
- Video: Musiba awataka Watanzania wasikubali kutumika
Aliongeza kuwa kiasi hicho cha fedha kitasaidia katika kutenga miradi ambayo haijihusishi na masuala ya dawa za kupunguza maumivu na kuhamamisha matumizi ya dawa za kupunguza maumivu sizizo na madhara.
Trump amesema kuwa anataka Marekani iwe taifa huru dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya.