Rais wa Marekani, Donald Trump ametangaza mkakati wake mpya wa kitaifa kuhusu masuala usalama utakaotumika katika utawala wake ambao utakuwa na kipaumbele cha Marekani kwanza.

Amesema kuwa mkakati huo umetilia mkazo katika suala la ukuaji wa uchumi na usalama wa taifa hilo, unatazamiwa kuweka sheria kali za kulinda mipaka na kuwa na jeshi imara.

Aidha, katika hotuba yake, Rais Trump amezitaja nchi za China na Urusi kuwa ni wapinzani wake wakuu wanaopinga ushawishi wa Marekani katika ngazi ya kimataifa.

Hata hivyo, ameongeza kuwa mkakati huo unajumuisha ujenzi wa ukuta katika mpaka wa Marekani na Mexico, ili kuweza kuimarisha sheria za uhamiaji na kusitisha mpango wa kutoa viza.

 

Manyanya awataka wataalam kubadilishana uzoefu
Vanessa Mdee: Maajabu mengi yametokea kwenye maisha yangu