Rais wa Marekani, Donald Trump ametoa vitisho vya kutaka kufunga mpaka wa Mexico endapo hawatafanya juhudi za kutosha kuzuia wahamiaji haramu wanaopitia mpaka huo kuingia USA.

Trump amefikia maamuzi hayo kufuatia kuongezeka kwa wahamiaji wanaopitia mpaka wa mexico na kuomba makazi Marekani.

Kwa upande wake, Rais wa Mexico, Andres Manuel amesema hataki kuhusishwa au kuingizwa kwenye suala hilo la Trump, na kuongeza kuwa suala la wahamiaji haramu sio la kulaumiwa nchi yao kwani nchi zinazofaa kutupiwa lawama ni za Amerika ya kati,

“wananchi wa Mexico hawatafuti tena kazi Marekani wahamiaji wengi sasa wanatokea nchi za Amerika ya kati” amesema Rais Manuel.

Trump amewaambia waandishi wa habari kuwa mpango mzuri unakuja kuhusiana na mpaka wa mexico wiki ijayo kwani walikuwa na uwezo wa kuwazuia wahamiaji haramu na hawaja amua kuchagua kufanya.

Nabaadaye akaendelea kuandika kwenye ukurasa wake wa ‘Tweeter’ kuwa wanapoteza pesa nyingi kwasababu ya Mexico hasa linapokuja suala la usafirishaji wa madawa ya kulevya, hivyo kufunga mipaka litakuwa jambo zuri la kufanya.

Kwamujibu wa Katibu wa ulinzi wa makazi ya ndani, Kirstjen Nielsen, amesema wahamiaji wanazidi kuongezeka kwa wingi ambao wanaomba makazi Marekani lakini tayari wamesha sababisha vurugu katika maeneo ya El Salvador, Honduras na Guatemala, na kuongeza kuwa kwa mwezi Machi wamepokea takribani wahamiaji haramu 100,000 idadi kubwa iliyovunja rekodi ya karne na jumla ya watoto 1, 000 wamechukuliwa na kuwekwa chini ya uangalizi.

kufungwa kwa mpaka wa Mexico na Marekani kutapelekea hatari ya kupata hasara za mabilioni ya dola yanayopatikana kutokana na biashara zinazohusisha mpaka huo.

Nandy aachia ngoma mpya, ''Halleluyah''
Video: Kigogo Takukuru aliyetajwa na JPM akosa dhamana, Nassari kukata rufaa ya Ubunge